1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG : Korea Kaskazini yashupalia msimamo wake wa nuklea

13 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbd

Korea Kaskazini kwa mara nyengine tena imesisitiza kwamba haki yake ya kuwa na mpango wa nuklea kwa ajili ya matumizi ya amani haistahiki kujadiliwa ikiwa ni masaa machache tu kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao ya nuklea mjini Beijing.

Mazungumzo hayo yanayozishirikisha nchi sita ambayo yanatarajiwa kuanza baada ya kuahirishwa kwa wiki sita yana lengo la kuishawishi serikali ya Pyongyang kuachana na tamaa yake ya kutengeneza silaha za nuklea.Mazungumzo hayo yalisitishwa hapo mwezi wa Augusti kutokana na madai ya Marekani kwa Korea Kaskazini kuiikongowa mitambo yake yote ya nuklea.

Korea Kaskazini ambayo mara kwa mara imekuwa ikiishutumu Marekani kwa kuwa hasimu na kukosa uaminifu inahudhuria mazungumzo hayo kwa kutaraji kunufaika kidiplomasia na kiuchumi ambako kutaweza kuisaidia nchi hiyo kupambana na baa la njaa ambalo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita limegharimu maisha ya watu milioni moja.