PYONGYANG: Korea Kazkazini yakataa kushirika katika mazungumzo hadi katikati ya mwezi ujao
29 Agosti 2005Matangazo
Korea Kazkazini imesema haitashiriki tena katika mazungumzo ya mataifa sita juu ya mpango wake wa nyuklia kabla ya katikati ya mwezi Septemba. Waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Paek Nam-Sun amewaambia waandishi habari mjini Pyongyang kwamba mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani na Korea Kusini yamevuruga mpango huo.
Mkutano wa sita juu ya mpango huo unaozijumulisha Korea Kusini, Korea Kazkazini, Marekani, Japan na Russia ulikwama mapema mwezi huu baada ya siku 13 za majadiliano.