PYONGYANG: Korea ya Kaskazini yajaribu makombora
26 Mei 2007Matangazo
Korea ya Kaskazini imefanya majeribo yake ya kwanza ya makombora baada ya kama mwaka mmoja. Waangalizi hii leo wamesema,majeribio hayo yametumiwa kama kuonyesha nguvu zake za kijeshi,ili kuzidi kuishinikiza Korea ya Kusini kuhusu msaada wa mchele.Serikali ya Seoul, inachelewesha kupeleka msaada wa tani 400,000 za mchele,mpaka Pyongyang itakapoanza kutekeleza makubaliano ya pande sita ya kusitisha mradi wake wa silaha za nyuklia.Seoul na Washington zilipuuza majeriibo yaliyofanywa siku ya Ijumaa na kusema lilikuwa zoezi la kawaida.