1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pyongyang. Korea yaamua kusitisha mpango wake wa kinuklia.

19 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZa

Korea ya kaskazini imesema kuwa iko tayari kusitisha kabisa mpango wake wa kinuklia.

Makubaliano hayo yamepatikana katika mazungumzo ya nchi sita mjini Beijing.

Katika taarifa ya pamoja , serikali ya Korea ya kaskazini pia imekubali kujiunga tena na mkataba wa kutosambaa kwa silaha za kinuklia na kusema itawaruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia katika maeneo yake ya shughuli za kinuklia.

Kutokana na hatua hiyo , Korea ya kaskazini itaruhusiwa kuendeleza shughuli zake za kinuklia kwa matumizi ya amani.

Mataifa mengine matano yanayoshiriki katika mazungumzo hayo Korea ya kusini , China, Japan , Russia na Marekani , pia yamesema yataipatia Korea ya kaskazini msaada wa nishati.