1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Majadiliano na Korea ya Kaskazini yaridhisha

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpX

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Christopher Hill amesema ameridhika na majadiliano yake na maafisa wa Korea ya Kaskazini.Alipozungumza na waandishi wa habari,Hill alisema majadiliano yalikuwa mazuri na yanakwenda mbele;na yanapaswa kusonga mbele.

Azma ya majadiliano hayo,ni kutekeleza makubaliano ya kusitisha mradi wa kutengeneza silaha za nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Hill ni afisa wa ngazi ya juu kabisa wa Marekani,kwenda Korea ya Kaskazini tangu miaka mitano iliyopita.

Katika mwezi wa Februari,Pyongyang ilikubali kukifunga kituo chake cha nyuklia cha Yongbyon, lakini si kabla ya kurejeshewa mamilioni ya Dola zake zilizokuwa zimezuiliwa katika benki ya Macau.Pesa hizo zilirejeshwa juma lililopita,na Korea ya Kaskazini imewaalika wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kurejea nchini humo baada ya kutokuwepo huko kwa muda wa miaka mitano.