Pyongyang. Majadiliano yanakwenda vizuri juu ya mpango wa kinuklia wa Korea kaskazini.
2 Septemba 2007Matangazo
Wajumbe wa ngazi ya juu wa majadiliano kutoka Marekani na Korea ya kaskazini wamesema kuwa wamepiga hatua katika siku ya kwanza ya mazungumzo yenye lengo la kusukuma mbele juhudi za kimataifa za kuzuwia mpango wa kinuklia wa nchi hiyo.
Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Chris Hill amesema kuwa amekuwa na mazungumzo yenye uwazi na ya kina juu ya jinsi Korea ya kaskazini itakavyosimamisha kabisa kinu chake cha kinuklia chini ya masharti ya makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya mataifa sita mapema mwaka huu.
Mwenzake wa Korea ya kaskazini , Kim Kye – gwan , amesema kuwa siku mbili za mwanzo za mazungumzo zimejumuisha majadiliano juu ya kuiondoa Korea ya kaskazini katika orodha ya mataifa yanayosaidia ugaidi.