1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Mamia ya watu wauwawa kwenye mafuriko

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZQ

Vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vimeripoti kwamba mamia kadhaa ya raia wameuwawa kufuatia mafuriko nchini humo.

Ripoti za awali zinasema nyumba zaidi ya 30,000 zimeharibiwa. Daraja na reli pia zimeharibiwa kufuatia mafuriko ya wiki nzima nchini humo.

Eneo lililoathirika zaidi ni mkoa wa Kangwon unaopatikana katika eneo la mpaka wa kusini wa Korea Kaskazini.