PYONGYANG. Mazungumzo ya pande sita juu ya silaha za nuklia yaanza tena
9 Novemba 2005Matangazo
Mazungumzo ya pande sita ya Korea kaskazini juu ya mpango wa silaha za kinuklia yameanza tena.
Pyongyang imesema kwamba Marekani imechangia kuzorota kwa mazungumzo hayo hasa baada ya ziara ya rais Bush huko Brazil na matamshi yake ya kumtaja kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong wa pili kama mtu dhalimu.
Hata hivyo bwana Kim Kye Gwan mpatanishi mkuu wa Korea Kaskazini ametabiri kuendelea vyema kwa mazungumzo hayo.
Washington inataka Pyongyang ibomoe kabisa mpango wake wa Nuklia lakini Korea Kaskazini inadai fidia kwanza kutoka kwa jamii ya kimataifa kabla haijatimiza azimio hilo.