PYONGYANG: Mgombea urais wa Marekani ziarani Korea Kaskazini
9 Aprili 2007Matangazo
Mgombea wadhifa wa urais nchini Marekani ambaye pia ni gavana wa jimbo la New Mexico, Bill Richardson, amewasili mjini Pyongyang, Korea Kaskazini.
Ziara ya gavana huyo wa chama cha Democratic na ujumbe wake inalenga kutafuta mabaki ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa wakati wa vita vya Korea katika miaka ya 1950.
Ziara ya gavana huyo nchini Korea Kaskazini imeidhinishwa na utawala wa rais George W Bush. Ziara hiyo pia inafanyika kabla muda uliowekewa Korea Kaskazini kukifunga kinu chake kikubwa cha nyuklia kumalizika Jumamosi ijayo kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya mataifa sita kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini mjini Beijing China.