1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Wakaguzi wa kinyuklia wamealikwa Korea Kaskazini

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrD

Korea ya Kaskazini imewaalika wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kujadili hatua ya kukifunga kituo chake kikuu cha nyuklia.Katika barua iliyowasilishwa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa -IAEA- serikali ya Pyongyang imesema,mgogoro wake wa pesa pamoja na Marekani uliokwamisha makubaliano ya kukifunga kituo cha nyuklia,sasa takriban umemalizika.Korea ya Kaskazini ilikataa kutimiza ahadi iliyotolewa mwezi wa Februari ya kukifunga kituo cha nyuklia, kabla ya kurejeshewa Dola milioni 25 zilizozuiliwa katika benki ya Macau.Marekani imeituhumu Banco Delta Asia kuwa imeisaidia serikali ya Korea ya Kaskazini kufanya bishara haramu ya pesa.Juma hili pesa zilizozuiliwa zilianza kupelekwa Korea ya Kaskazini.