Pyongyang. Wanajeshi wa Korea ya kaskazini waingia katika eneo lililopigwa marufu.
7 Oktoba 2006Matangazo
Wanajeshi wa Korea ya kusini wamefyatua risasi za tahadhari baada ya wanajeshi watano wa Korea ya kaskazini kwa muda kuvuka mpaka na kuingia ndani ya eneo la kusini la eneo ambalo halitakiwi kuwa na wanajeshi ambalo linatenganisha nchi hizo mbili.
Wakuu wa vikosi vya jeshi la Korea ya kusini wamesema katika taarifa kuwa wanajeshi hao wa Korea ya kaskazini walipindukia katika mstari wa unaotenganisha majeshi hayo licha ya kutolewa onyo mara kwa mara kupitia vipaza sauti.
Taarifa hiyo imesema kuwa wanajeshi hao waliingia kiasi cha mita 30 katika eneo hilo lakini walirejea baada ya risasi kufyatuliwa.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa.