1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Wito kujadiliana uso kwa uso na Marekani

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjE

Jeshi la Korea ya Kaskazini limetoa wito wa kufanywa mazungumzo ya ana kwa ana pamoja na Marekani.Hati iliyotolewa na jeshi la Pyongyang imesema,mazungumzo hayo yatahusika na masuala ya kuhakikisha amani na usalama wa Rasi ya Korea. Hivi karibuni,Marekani iliashiria kuwepo tayari kufanya mazungumzo ya kurekebisha uhusiano na pia kujadili mkataba wa amani wa kumaliza rasmi Vita vya Korea;lakini mambo hayo yanahusishwa na suala la Korea ya Kaskazini kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia.Tume ya wataalamu wa Shirika la la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa-IAEA, inatazamiwa kuwasili Korea ya Kaskazini siku ya Jumamosi.Tume hiyo itasimamia utaratibu wa kufunga mtambo wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini, unaozalisha plutonium ambayo huweza kutumiwa kutengenezea silaha.