1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pyongyang.Korea ya kaskazini yataka mazungumzo na Korea ya kusini.

14 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDl

Korea ya kaskazini imependekeza kufanya mkutano na Korea ya kusini mapema wiki ijayo. Pendekezo hilo la kuwa na mkutano huo limekuja katika ujumbe uliotumwa kutoka Korea ya kaskazini kwenda kwa waziri wa masuala ya muungano wa Korea ya kusini leo Jumamosi.

Wizara hiyo imesema itatumia mkutano huo kuishinikiza Korea ya kaskazini kurejea katika meza ya majadiliano kuhusiana na shughuli zake za masuala ya kinuklia.

Korea zote mbili, Marekani, Japan, China na Russia zilikutana kwa duru tatu za mazungumzo hadi Juni 2004 ambapo hakukuwa na maendeleo yaliyopatikana.

Korea ya kaskazini imekubali kukutana kwa mara ya nne, katika mkutano uliopangwa kufanyika Septemba mwaka jana, lakini hadi sasa mkutano huo haujafanyika.