1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG:Mkutano wa nchi sita juu ya mpango wa Nuklia wa Korea Kaskazini kuendelea

31 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEp7

Wapatanishi kutoka mataifa sita wanaendelea kujaribu kuichambua taarifa ya pomaoja juu ya mpango wa Korea kaskazini wa kutengeneza silaha za Nuklia.

Mazungumzo hayo muhimu yakiingia siku yake ya sita hii leo mjini Beijing yanaonekana kuelekea kuzorota.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa na China inataka kuwepo njia ya kuelekea mbele kwa mazungumzo hayo yaliyochukua muda wa miaka miatatu bila mafanikio .

Lakini hata hivyo mzozo uliobakia kwa sasa ni juu ya masharti ya Korea Kaskazini iwapo itaamua kuachana na mpango wake huo wa Nuklia.Baada ya saa kadha za majadaliano makali mikutano mingine imepangiwa kufanyika hapo kesho.