1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raila Odinga amtaka Kibaki ajiuzulu

10 Februari 2008

Matamshi yanaondoa uwezekano wa kupatikana mwafaka wa kisiasa

https://p.dw.com/p/D58p

NAIROBI

Kiongozi wa upinzani wa chama cha ODM Raila Odinga amemtaka rais Kibaki ajiuzulu na uchaguzi mwingine ufanyike matamshi ambayo yanatilia mashaka tangazo lililotolewa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa kwamba viongozi wa kisiasa wanaopingana wanakaribia uwezekano wa kufikia suluhu ya kisiasa kuhusu mgogoro wa uchaguzi.Raila Odinga ameyatoa matamshi yake jana jumamosi katika eneo la magharibi katika mkusanyiko wa maziko ya mbunge wa chama chake David Kimutai Too aliyeuwawa na afisa wa polisi hivi karibuni.Maelfu ya wafuasi wa chama cha ODM waliohudhuria maziko hayo walishangiria matamshi hayo ya bwana Odinga.

Ijumaa iliyopita katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan ambaye anaongoza juhudi za amani kati ya serikali na upinzani nchini humo alitangaza kwamba pande zote mbili zimekubaliana kwamba kuna haja ya kupatikana suluhisho la kisiasa na hivyo kutoa matumaini mema kwamba huenda pande hizo mbili zikafikia uamuzi wa kuunda serikali ya pamoja pengine wiki ijayo lakini sasa msimamo huo wa bwana Raila uliojitokeza tena huenda ukayaondoa matumaini hayo.