Biden akutana na mwenzake wa Poland na kuahidi mshikamano
21 Februari 2023Matangazo
Akihutubia mkutano na waandishi habari baada ya mazungumzo yake na rais Duda, Biden amesema bara la Ulaya ni lazima libakie kuwa salama na mshikamano wa mataifa ya magharibi umezidi kuimarika tangu Urusi ilipoanzisha vita nchini Ukraine.
Kwa upande wake rais Duda ameusifu msimamo wa Biden ikiwa ni pamoja na ziara aliyoifanya jana mjini Kyiv kuonesha mshikamano na Ukraine.
Baadaye leo jioni rais Biden atatoa hotuba inayotarajiwa kuzungumzia pamoja na mambo mengine msimamo usioyumba wa mataifa ya magharibi katika kuiunga mkono Ukraine kwenye vita dhidi ya Urusi.