Rais Macron amteua Francois Bayrou kuwa Waziri Mkuu mpya
13 Desemba 2024Bayrou mwenye umri wa miaka 73 na kiongozi wa chama cha siasa za mrengo wa kati cha Democratic Movement (MoDem), anakabiliwa na changamoto ya kuwashawishi wabunge kuhusu kupitishwa kwa bajeti ya mwaka ujao na ameeleza kuhusu ugumu wa nafasi hiyo.
" Nadhani kila mtu anaelewa ugumu wa kazi hii. Nadhani kila mtu pia anafikiria kuwa kuna njia inayotakiwa kupatikana, ambayo itawaunganisha watu badala ya kuwagawanya. Na huu ni wakati mzuri kwa sababu leo sherehe ya kuzaliwa ya mfalme wa Ufaransa Henry wa IV, ambaye niliandika mno kumhusu kwa sababu nadhani maridhiano yanahitajika,” amesema Bayrou.
Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Nationa Rally Marine Le Pen amesema Bayrou anapaswa kuvisikiliza vyama vya upinzani ili kuunda mpango wa bajeti ulio bora.
Kwa upande wake kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti Olivier Faure, ametangaza kuupinga waziwazi uteuzi wa Francois Bayrou kama waziri Mkuu mpya wa Ufaransa.