1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron awasili Mayotte kutathmini uharibifu wa kimbunga

19 Desemba 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili Mayotte kutathmini uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Chido kwenye visiwa vya Bahari ya Hindi, wakati shughuli za uokozi na kusambaza misaada zikiendelea kushika kasi.

https://p.dw.com/p/4oLlp
Kimbunga Chido kisiwani Mayotte
Idadi ya vifo vya kimbunga hicho kibaya zaidi kutokea katika historia ya eneo hilo vinaweza kufikia mamia au maelfuPicha: Adrienne Surprenant/AP Photo/picture alliance

Ziara yake katika eneo hilo linalomilikiwa na Ufaransa inakuja baada ya jana Jumatano usiku serikali kutangaza "hatua za kipekee za janga la asili" kwa Mayotte ili kuwezesha "usimamizi mzuri zaidi wa kukabiliana na janga".

Soma pia: Ufaransa yaendelea kupeleka misaada Mayotte baada ya kimbunga

Maafisa wameonya kwamba idadi ya vifo kutokana na kimbunga hicho kibaya zaidi kutokea katika historia ya eneo hilo vinaweza kufikia mamia au pengine maelfu katika wakati ambao waokoaji wapo katika kazi ya kuondoa vifusi kwenye mitaa ya mabanda ili kutafuta manusura.

Soma pia:Waliofariki kwa Kimbunga Chido Msumbiji wafikia 45

Idadi ya awali kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa inaonyesha kuwa watu 31 wamethibitishwa kufa, 45 kujeruhiwa vibaya, na zaidi ya 1,370 wakiuguza majeraha.