1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin ziarani Ujerumani

8 Aprili 2013

Ziara ya rais Putin nchini Ujerumani, kishindo kinachomkumba mwendesha mashtaka katika kesi ya rais wa zamani Christian Wulff na Bayern Munich kunyakua taji hata kabla ya mwisho wa michuano ya Bundesliga magazetini

https://p.dw.com/p/18BeT
Rais wa Urusi Vladimir Putin na kansela Angela Merkel wakijibu masuala ya waandishi habari katika maonyesho ya viwanda mjini HannoverPicha: Reuters

Tuanze lakini na uhusiano kati ya Ujerumani na Urusi. Gazeti la Straubinger Tagblatt/Landshuter Zeitung linaandika:Uhusiano kati ya Ujerumani na Urusi mtu anaweza kusema unadorora. Putin, akiringia utajiri mkubwa wa mali ghafi wa nchi yake kubwa kupita kiasi, anafuata sera zake mwenyewe za dola kuu linalojinata-anavutiwa na hali ya maisha na vitega uchumi vya nchi za magharibi lakini hataki nasaha wala onyo. Zaidi ya hayo Ulaya, kutokana na kukabwa na mgogoro wa kiuchumi na fedha haina cha kuiambia Urusi badala ya maneno.

Gazeti la "Lausitzer Rundschau" linaandika:Tathmini ya Putin kuhusu madaraka ndiyo inayofuja hali ya kuishi pamoja.Uchumi wa Urusi unakua, idadi ya wasiokuwa na kazi ni ndogo na bajeti inalingana na mapato ya nchi. Lakini yote hayo yasituhadae tukasahau kwamba demokrasia inatoweka,makampuni yanaanza upya kutaifishwa,umangimeza,na rushwa vinakithiri-kwa mtazamo wa muda mrefu,yote hayo sio tuu yataufanya upooze uhusiano wa kirafiki, bali pia yatageuka kuwa kitisho kwa wateja na washirika.Kwa hivyo Angela Merkel na Vladimir Putin watakuwa na mengi ya kuzungumzia na sio pekee kuhusu kuvamiwa wakfu wa Ujerumani nchini Urusi .

Eti kweli kaonewa?

Christian Wulff Ex-Bundespräsident ARCHIV Juli 2012
Rais wa zamani wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Christian WulffPicha: picture-alliance/dpa

Mahakama ya mjini Hannover inatarajiwa kuamua hii leo kama itamfungulia mashtaka au la rais wa zamani wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Christian Wulff kwa madai ya kupokea hongo. Christian Wulff amekataa hapo awali kulipa faini ya Euro 20 000 ili kesi yake iweze kusitishwa. Anadai hana hatia na anataka badala yake atakaswe na madai yote dhidi yake. Gazeti la Nürnberger Zeitung linaandika:"Yadhihirika kana kwamba mwendesha mashtaka anapendelea zaidi kuifunga moja kwa moja tena bila ya makelele kesi hiyo. Kinyume lakini na mtuhumiwa. Bila ya shaka hukmu ya "hana hatia" itazusha suala kama yote yaliyotokea hayakuwa mbinu za kumtimua madarakani mtu ambae hakufanya kitu - kwa sababu kujiuzulu Christian Wulff kama rais wa shirikisho hakujasabbishwa na chengine isipokuwa kisa cha kufunguliwa mashtaka tu. Yeye binafsi aliwahi wakati mmoja kusema "sio yote ni barabara hata kama hayaandamiwi kisheria. Hata hivyo ni jambo la kusikitisha kwa mtu ambae wakati mmoja alikuwa kileleni, awe hapatiwi fursa ya pili.

Taji la 23 la ligi kuu kwa Bayern Munich

Bundesliga 2013 Fußball München Fans
Mashabiki wa timu ya Bayern Munich wakisherehekea ushindi wa timu yao dhidi ya Eintracht Frankfurt na kutwaa kwa mara ya 23 na kabla ya wakati taji la ubingwa wa ligi kuuPicha: picture-alliance/dpa

Na hatimae gazeti la Donaukurier linaandika kuhusu Bayern Munich kutwaa taji la ubingwa hata kabla ya michuano ya ligi kuu kumalizika. Gazeti linaendelea kuandika.Bayern Munich ndio mabigwa wa ligi kuu.Hii ni mara ya 23.Ukiwa shabiki wa dimba huna budi kuwapongeza-Inafurahisha jinsi mbinu na mkakati wao ulivyofanikiwa.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Khelef