Rais Tinubu awasilisha bungeni miswada muhimu ya kodi
6 Desemba 2024Matangazo
Mageuzi hayo yameibua upinzani mkali, yakidhihirisha mvutano wa muda mrefu katika nchi hiyo iliyogawika mara mbili, eneo la kaskazini lenye Waislamu wengi na upande wa kusini wenye Wakristo wengi.
Miswada hiyo ya kodi inalenga kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuifanya nchi hiyo, inayotegemea mafuta kwa asilimia kubwa kama chanzo kikuu cha mapato yake, kuwa kivutio bora kwa wafanyibiashara wa ndani na wawekezaji wa kigeni.
Tinubu aahidi kushughulikia madai ya raia
Iwapo miswada hiyo itapitishwa na kuwa sheria, itapunguza ushuru unaotozwa watu binafsi na wanafanyibishara, na pia kupunguza kodi za mapato ya makampuni kutoka asilimia 30 hadi 25 katika muda wa miaka miwili ijayo.