1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Uhuru azuru ngome ya mpinzani wake Raila

Josephat Nyiro Charo19 Aprili 2013

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, leo amezuru mji wa Kisumu, ngome kuu ya mpinzani wake mkuu katika uchaguzi wa rais wa mwezi Machi, waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga.

https://p.dw.com/p/18JcX
epa02623841 (FILE) A file photo dated 15 December 2010 shows Kenya's Finance Minister and Deputy Prime Minister Uhuru Kenyatta arriving at a press conference on the day the International Criminal Court (ICC) announced six prominent Kenyans, which included Kenyatta, who are said to be responsible for masterminding the country's 2007/08 post-election violence that left some 1,300 dead. According to a local report, five suspects, Kenyatta, former higher education minister William Ruto, suspended Industrialisation Minister Henry Kosgey, former police commissioner Maj-Gen Hussein Ali, and Head of Operation at KASS FM radio Joshua Arap Sang said on 09 March 2011 that they will honor summonses issued for the charges of crimes against humanity by the pre-trial chamber of the ICC. The sixth suspect is the Secretary to the Cabinet and Head of the Civil Service Francis Muthaura. EPA/DAI KUROKAWA
Kenia Uhuru KenyattaPicha: picture-alliance/dpa

Uhuru amefanya ziara yake hiyo ambayo ni kwanza nje ya mji mkuu Nairobi, kuhuduria mazisho ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama waalimu nchini humo, David Okuta. Rais Uhuru na waziri mkuu Raila Odinga walikuwa miongoni mwa mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya aliyekuwa kaibu mkuu wa chama cha waalimu nchini Kenya, David Okuta, katika jimbo la Kisumu.

Shughuli ya maziko hayo imefanyika katika shule ya msingi ya Onjiko, karibu na nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Tura. Rais Uhuru aliwasili mwendo wa saa tano na nusu kutumia helikopta ya jeshi. Raila naye aliwasilia muda mfupi baadaye.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo ya mazishi rais Uhuru amesema, "Na mimi nataka niwahakikishie nyote ya kwamba serikali sio serikali ya sehemu hii au ya watu wale. Serikali ni ya taifa la Kenya na wananchi milioni 40 ambao wanaishi katika taifa letu la Kenya." Uhuru aidha amesema anatarajia kufanya kazi pamoja na viongozi wote, akiwemo Raila Odinga, ambaye amemueleza kuwa ni kakake, ili kuhakikisha wanaliunganisha taifa la Kenya, kutimiza ahadi walizitoa, na kuyainua maisha ya Wakenya.

Raila Odinga, Prime Minister of Kenya, makes a point at a session called, "More voting, less Democracy", during the second day of the World Economic Forum on Africa on May 5, 2011, in Cape Town, South Africa. African economies are among the world's fastest-growing but leaps in output have not been a silver bullet for better living standards, delegates at the World Economic Forum said Thursday. AFP PHOTO/RODGER BOSCH (Photo credit should read RODGER BOSCH/AFP/Getty Images)
Waziri mkuu wa zamani wa Kenya, Raila OdingaPicha: RODGER BOSCH/AFP/Getty Images

Uhaba wa waalimu Kenya

Raila kwa upande wake amesema Kenya inakabiliwa na uhaba mkubwa wa waalimu. "Kwa sababu tunafahamu tuna upungufu mkubwa sana wa waalimu. Tunahitaji waalimu 80,000 zaidi ili kupunguza pengo kati ya mwalimu na mwanafunzi nchini mwetu, ili kuboresha ubora wa utoaji mafunzo. Nadhani hili ni suala tunalohitaji kulishuhgulikiwa kadri tunavyozungumzia jinsi ya kuboresha mazingira ya waalimu kufanyia kazi."

Akijibu hoja hizo rais Uhuru ameahidi kwamba serikali yake itashirikiana na viongozi wa vyama vya waalimu nchini kwa masilahi ya waalimu, wanafnzi na wananchi wote kwa ujumla.

Usalama uliimarishwa katika eneo hilo huku idadi kubwa ya maafisa wa usalama wakitumwa kupiga doria, wakiwemo maafisa wa kikosi cha kupambana na fujo cha GSU. Maafisa hao waliwafanyia upekuzi waombolezaji katika lango la shukle hiyo, huku maafisa wa GSU wakiwekwa kushika doria kila upande wa barabara ya mita 200 inayoelekea katika shule hiyo, kutoka barabara ya Ahero kwenda Kericho. Helikopta ya jeshi la polisi ilionekana ikizunguka anga ya eneo hilo.

Mwili wa marehemu ulisindikiwa katika shule hiyo kutoka nyumbani kwake na bendi ya jeshi la polisi, dakika chache baada ya saa nne asubuhi. Okuta, aliyekuwa na umri wa miaka 61, aliaga dunia wiki mbili zilizopita katika hospitali moja ya mjini Nairobi, ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua nyumbani kwake. Amewaacha wajane wawili na watoto wanane. Mamia ya waalimu wamehudhuria mazishi hayo, wengi wao wakisafirishwa kwa mabasi hadi eneo hilo.

Mwandishi: Josephat Charo/PPS, Kenya

Mhariri: Mohamed Khelef