1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto akiri ukiukaji wa polisi katika maandamano

1 Januari 2025

Rais wa Kenya William Ruto amekiri ukiukaji uliofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo, kufuatia maandamano ya kupinga wimbi la hivi majuzi la madai ya utekaji nyara ambayo yamezua ghadhabu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4ojDT
Rais | William Ruto Mahojiano na DW
Rais wa Kenya William RutoPicha: DW

Ruto amesema kwenye hotuba yake ya mwaka mpya kuwa kumekuwepo na matukio ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na ya kinyume cha sheria yaliyofanywa na polisi. Hata hivyo hakufafanua ni vitendo vya aina gani.

Soma pia: Hasira zaongezeka Kenya kuhusiana na utekaji wa wakosoaji 

Kiongozi huyo amesema kuwa ni muhimu kukumbuka kwamba kila uhuru una ukomo, na usalama wa umma na utaratibu wa sheria lazima vizingatiwe kwanza kabla ya uhuru wa mtu yeyote.

Vikosi vya usalama vya Kenya vinatuhumiwa kwa kuwashikilia watu kadhaa kinyume cha sheria tangu maandamano ya kuipinga serikali yaliyoongozwa na vijana mwezi Juni na Julai yalipokandamizwa vikali.