1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Korea ya kusini ziarani nchini Ujerumani

12 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFO0

Berlin:

Ujerumani inaunga mkono juhudi za Korea ya kusini za kujongeleana na Korea ya kaskazini ya kikoministi.Rais wa shirikisho Horst Köhler amesema hayo wakati wa karamu iliyoandaliwa kwa heshma ya kiongozi mwenzake wa Korea ya kusini ROH MOO HYUN mjini Berlin."Serikali ya mjini Seoul inaweza kutegemea ushirikiano wa kisiasa hasa linapohusika suala la kuponesha majaraha yaliyosababishwa na miongo kadhaa ya mtengano."Rais Roh amesifu uhusiano wa dhati ulioko kati ya nchi hizi mbili akisema Ujerumani inaendelea kuwa mfano mzuri wa kuigizwa nchini mwake.Kabla ya hapo viongozi hao wawili walizungumzia juu ya mradi wa kinuklea wa Korea ya kaskazini, na hali nchini Irak.Rais wa Korea ya kusini ataondoka Ujerumani alkhamisi ijayo kuelekea Uturuki.