Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ahimiza umoja
24 Desemba 2024Katika hotuba hiyo anayoitoa siku moja kabla ya sikukuu ya krismasi amezungumzia shambulio la hivi karubuni katika masoko ya krismasi katika mji wa Mashariki mwa Ujerumani wa Magdeburg. Ameziambia familia zilizoathirika kwamba haziko peke yao katika hili na kwamba taifa linasimama nao na kuomboleza nao wakati huu mgumu.
Steinmeier, pia aliwapongeza maafisa wa usalama na wataalamu wa afya kwa kazi yao kubwa baada ya shambulio hilo, akitoa wito zaidi kwa wajerumani kutogawanywa na matukio haya akisema chuki na vurugu havipaswi kupewa nafasi katika jamii.
Ijumaa ya tarehe 20 Desemba mwanamume mmoja mwenye asili ya Saudi Arabia aliyetambuliwa kwa jina la Taleb A, alivurumisha gari katikati ya umati wa watu kwenye soko la Krismasi na kusababisha mauaji ya watu 5 na wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa.