1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Emmerson Mnangagwa ashinda awamu nyingine

27 Agosti 2023

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amechaguliwa kuiongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

https://p.dw.com/p/4VcRx
Zimbabwe inatambulika kwa uchaguzi ambao hugubikwa na mashaka ya udangaynifu.
Rais wa Zimbabwe emmerson Mnangagwa amechaguliwa kuongoza kwa awamu nyingine ya miaka mitano Picha: Jekesai Njikizana/AFP via Getty Images

Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kumpa ushindi Emmerson Mnangagwa yametangazwa Jumamosi usiku, mapema kuliko ilivyotarajiwa katika taifa hilo lenye historia ya vurugu na mizozo wakati wa uchaguzi.

Ushindi wa Mnangagwa unamaanisha kuwa chama cha ZANU-PF kinaendelea kushika dola. ZANU-PF kimeongoza kwa miaka yote 43 tangu Zimbabwe ilipopata uhuru  mwaka 1980, chini ya marais wawili ambao ni hayati Robert Mugabe na Emmerson Mnangagwa.

Msemaji wa moja ya chama cha upinzani aliyezungumza muda mfupi baada ya Mnangagwa kutangazwa mshindi kwa asilimia 52.2 alisema wangeyapinga matokeo kwa kuwa "yalikusanywa kwa haraka bila kuhibitishwa kwa usahihi".