1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON: Gambari arejea Burma kuzungumza na serikali

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AC

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari amerejea Burma kwa mazungumzo ya pili pamoja na viongozi wa kijeshi waliotumia nguvu,kuzuia maandamano ya watawa wa Kibudha katika mwezi wa Septemba.Ziara hiyo lakini imegubikwa na uamuzi wa utawala wa kijeshi,kumfukuza Charles Petrie aliekuwa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Burma.

Gambari pia anatazamia kukutana na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi anaezuiliwa kutoka nje ya nyumba yake.Chama chake cha „National League for Democracy“ kilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 1990 lakini hakuruhusiwa kushika madaraka.