1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rangoon. Watoto wanaandikishwa jeshini Burma: Ripoti inasema.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7B3

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema kuwa jeshi la Burma linawalazimisha watoto kutumikia jeshi hilo. Ripoti iliyotolewa na shirika hilo lenye makao yake makuu mjini New York imesema kuwa watoto wengine wakiwa na umri wa miaka 10 wanapigwa ama kutishiwa kukamatwa ili kuwafanya wakubali kujiunga na jeshi.

Ripoti hiyo inasema kuwa jeshi la Burma limekuwa likiwaandikisha kwa nguvu watoto ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka ya wanajeshi wapya kutokana na kuzidi kupanuka kwa jeshi, idadi kubwa ya wanajeshi wanaokimbia jeshi na ukosefu wa watu wazima wanaojitolea kujiunga na jeshi. Ripoti hiyo inatoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka vikwazo ikiwa ni pamoja na vikwazo vya silaha dhidi ya utawala wa kijeshi wa Burma.