1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ribery anungunika Bayern Munich

3 Machi 2009

Na Alex Ferguson adai Manchester United bado haijavaa taji.

https://p.dw.com/p/H4tI
Franck Ribéry.Picha: pa / dpa

Wakati kocha wa mabingwa wa Uingereza Manchester United,Sir Alex Ferguson, awaonya wachezaji wake wasihadaike kudhani wameshavaa taji la Premier League, stadi wa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, mfaransa Franck Ribery,awakosoa wachezaji wenzake kuwa hawamsaidii uwanjani huku fununu zikienea kwamba ,klabu nyengine zapiga hodi mlangoni mwake kumtaka ajiunge nazo.

Stadi wa timu ya taifa ya Ufaransa,Franck Ribery,ndie injini ya hujuma za Bayern Munich,mabingwa wa Ujerumani .Lakini hata gurudumu nalo kuna wakati linachoka kuzunguka.Robery,amewakosoa wachezaji wenzake kuhusu mbinu wanazotumia uwanjani-kwa muujibu vyombo vya habari vya Ujerumani vilivyoripoti jana.

"Nimelalamika kwa kocha Klinsmann kuwa sipewi msaada wa kutosha na wenzangu ninapokwenda kuhujumu upande wa shoto." Robery aliliambia gazeti la BILD akaongeza "na kocha Klinsmann alisema ananiungamkono hapo."

Ribery mara nyingi ambae akitajwa kujiunga na klabu nyengine kwa kitita kikubwa cha fedha akizungumzia hapo m cehzo wa kuvunja moyo wa juzi jumapili pale Munich ilipomudu sare ya 0:0 na Werder Bremen,licha ya kuwa Bremen tangu takika ya 15 ya mchezo ikicheza na wachezaji 10 ujwanjani.

tuhuma zake hizo Ribery zimechomoza wsakati ambapo kuna uvimu juu ya hatima yake katika Bayern Munich .Taarifa za hivi punde zasema huenda Franck Ribery,akahamia La Liga-ligi ya spian.Hasa akajiunga na klabu ya jogoo la Kamerun,Samuel Eto-o, FC Barcelona -viongozi wa Ligi.

Hata Franz Beckenbauer, rais wa Bayern munich amefadhahishwa na hali ya mambo inayomkuta Ribery.Alisema,

"Daima ni tatizo pale mchezaji akitaka kuiachamkono timu na anaitia shindo timu yake kwavile nafasi za kuondoka ni ndogo."

Alisema Beckenbauer.Wakati wa likizo za majira ya baridi,Franck Ribery alizusha balaa huko Munich aliposema ingekuwa ni ndoto yake kujiunga na hasimu wa FC Barcelona-Real Madrid.

Nae kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amewaonya wachezaji wake wasidhani kwamba tayaru wamelitia taji la ubingwa wa Uingereza kapuni.Alibashiri kwamba, Manu itapoteza pointi mwezi ujao wa April.

Manu imekamilisha daraja ya pili ya mradi wake wa kutwaa mataji 5 msimu huu kwa kulinyakua kombe la Liogi uwanjani wembley jumapili ,wana changamoto na New Castle hapo kesho.wanaweza hapo kufungua mwanya wa pointi 4 kileleni mradi Chelsea imetamba tu mbele ya portsmouth na Liverpool mbele ya Middlesbrough.

Kocha mpya wa Chelsea,Guus Hiddink anaendelea kuwapa matumaini Chelsea kwsamba waweza kuwatia munda Manchester na kuvaa wao taji msimu huu.Na Sir Alex Ferguson, anamuungamkono Hiddink kwa kupalilia zaidi matumaini madogo walionayo Chelsea kuweza kutwaa taji.