1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Dunia itakuwa na watu wanene kupita kiasi 2035

2 Machi 2023

Zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani itakuwa na uzito wa mwili kupita kiasi ifikapo mwaka 2035 ikiwa hatua muhimu hazitochukuliwa.

https://p.dw.com/p/4OAMN
Symbolbild Ernährung & Übergewicht
Picha: Dominic Lipinski/empics picture alliance

Hayo ni kulingana na ripoti mpya iliyotolewa mwaka huu na shirikisho la kimataifa la kupambana na unene uliyopindukia.

Shirikisho hilo linatabiri kuwa asilimia 51 ya watu duniani, ambao ni zaidi ya watu bilioni 4, watakuwa na unene au uzito kupita kiasi ndani ya miaka 12 ijayo.

Viwango vya watu wenye unene kupindukia vinaongezeka haraka mno miongoni mwa watoto na katika nchi zenye kipato cha chini.

Akizielezea takwimu hizo kama "onyo lililo wazi", Louise Baur, Rais wa Shirikisho la Watu Wanene Duniani, amewataka viongozi wenye jukumu la kutunga sera, kuchukua hatua sasa ili kuzuia hali hiyo inayozidi kuwa mbaya.