1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF yasema imechukua udhibiti kaskazini mwa Darfur

23 Desemba 2024

Kundi la wanamgambo wa RSF nchini Sudan limetangaza kuchukua udhibiti kwa mara nyingine wa eneo muhimu la kusafirisha na kupokea mizigo la Darfur Kaskazini hapo jana Jumapili.

https://p.dw.com/p/4oVKk
Sudan Omdurman 2024 |  Anhaltende Kämpfe
Washiriki wa wakuu wa timu ya kutegua mabomu huko Omdourman mnamo Novemba 2, 2024.Picha: Amaury Falt-Brown/AFP

Hatua hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya eneo hilo kuchukuliwa na vikosi hasimu vinavyoshirikiana na jeshi la Sudan. Hapo awali jeshi la Sudan na vikosi vinavyoshirikiana nalo vilisema katika taarifa ya pamoja kwamba walichukua udhibiti wa kituo cha cha al-Zurug ambacho RSF imekitumia tangu kuanza kwa vita kama eneo la msingi la kupata vifaa kupitia mipaka ya nchi jirani za Chad na Libya. RSF imevishutumu vikosi hasimu kwa kuwaua raia na kuchoma moto nyumba za maeneo jirani na kuharibu huduma za umma wakati wa uvamizi huo. Wachambuzi wanaofuatilia mzozo huo wanasema tukio hilo linaweza kuongeza uhasama baina ya vikosi vya RSF na vikosi hasimu vinavyoliunga mkono jeshi la serikali. Mzozo kati ya RSF na jeshi ulianza mwezi Aprili 2023, na mapigano makali yamekuwa yakishuhudiwa katika eneo la Darfur Kaskazini ambako kuna kambi za vikosi mbalimbali vya kijeshi