1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rushwa bado ni tishio kwa Ethiopia

Admin.WagnerD21 Juni 2013

Ethiopia inaweza kuwa moja ya nchi zisizotoa mafuta barani Afrika ambayo uchumi wake umekuwa haraka katika miaka ya hivi karibuni, lakini rushwa katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika imekuwa tishio kwa wawekezaji wa nje

https://p.dw.com/p/18u3L
Waziri mkuu wa Ehiopia Haile Mariam Desalegn
Waziri mkuu wa Ehiopia Haile Mariam DesalegnePicha: CC-BY-SA- World Economic Forum

Rushwa inatoa kitisho kwa sababu huyafanya masoko ya ndani kutokuwa na ushindani, yasiotabirika na hivyo kutoa sura mbaya kwa wawekezaji wa muda mrefu. Hayo ni maoni ya mchambuzi wa masuala ya Afrika mashariki katika Shirika linalochunguza masuala aa kisiasa la Afrika Risk Consulting, Ed Hobey.

Mei 11 mwaka huu katika hatua kubwa kabisa ya kupambana na rushwa, isiyowahi kushuhudiwa nchini Ethiopia kwa miaka 10, maafisa waliwakamata zaidi ya watu maarufu 50 wakiwemo maafisa wa serikali, wafanyabiashara na waziri mmoja.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya forodha na mapato Melaku Fanta, ambaye wadhifa wake ni sawa na Waziri, Naibu wake Gebrewahid Woldegiorgis na maafisa wengine walitiwa nguvuni kwa kushukiwa kwamba wamekiuka ulipaji kodi. Lakini kukamatwa kwao kumezusha hoja juu ya kiwango cha rushwa katika moyo wa wanasiasa vigogo nchini humo.

Berhanu assefa kutoka tume ya amaadili na kupambana na rushwa nchini humo, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kukamatwa watu hao kunaashiria jinsi rushwa ilivyoingia hadi katika ngazi za juu za uongozi.

Alisema, rushwa ni tatizo kubwa wanalokabiliana nalo. Na kwamba sasa wanashuhudi ikizagaa hadi nafasi za juu kuliko walivyotarajia. Sekta zilizokumbwa ni usimamizi wa ardhi, kodi na mapato, sheria, mawasiliano, maeneo ya umilikaji ardhi na leseni na sekta ya fedha.

Ethiopia iko nafasi ya 113 kati ya nchi 176 kwenye orodha ya Shirika la kupambana na rushwa la kimataifa, ambao ni muungano wa jumuiya za kiraia duniani unaopigania kuweko na uwajibikaji. Nchi hiyo ya pembe ya afrika, pia imepoteza dola bilioni 12 tangu mwaka 2000 kutokana na fedha zinazovushwa nje ya nchi kinyume cha sheria - hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa taasisi ya kimataifa ya masuala ya fedha na uadilifu, ambayo takwimu zake zinategemea maelezo rasmi yaliotolewa na serikali ya Ethiopia kwa Benki ya dunia na Shirika la fedha la kimataifa IMF.

Profesa wa Uchumi katika chuo cha Harper nchini Marekani Getachew Begashaw aliliambia Shirika la habari la IPS kwamba kulikuawa na wasiwasi kwamba kukamtawa kwa vigogo hivi karibuni ni mchezo tu wa kisiasa uliolengwa kuwafurahisha wafadhili wakubwa kama Benki ya dunia na Shirika la fedha la kimataifa na kuipa sifa serikali mpya kwamba inapambana na rushwa.

Waziri mkuu Hailemariam Deasalegn alichukua hatua za uongozi wa nchi kutoka kwa hayati Waziri mkuu Meles Zenawi aliyefariki dunia Agosti 22. Chama cha ukombozi wa Tigray TPLF ni mshirika mkuu katika muungano unaotawala wa EPDRF. Hata hivyo Watigray ni 8 tu asili mia ya wakaazi milioni 90 wa Ethiopia.

Kwa mujibu wa mwandishi habari Abebe Gellaw anayeishi uhamishoni na muanzilishi wa mtandao sauti ya Addis unaotoa habari ambazo huchujwa na serikali ya Ethiopia, ni kwamba makampuni yanayoendesha na kundi la wafanyabiashara linaloitwa fuko la ujenzi mpya wa Tigray linachukua akaribu nusu aya uchumi na liko karibu ana muungano unaoatawala. Fuko hilo limegeuka la kibiashara kwa ajili ya vigogo wakitigray ambao wanamiliki maeneo muhimu ya kiuchumi.

Ili kupambana kidhati na rushwa, wakosoaji wanasema, pamoja na mambo mengi yanahitajika mageuzi katika sekata ya forodha na serikali iwe na uwazi zaidi. Jumuiaya ya kimataifa pia inaweza kutoa mchango kwa kuhakikisha inapatiwa taarifa kuhusu utaratibu wa kukuasanya kodi ili kuufanya kuwa mgumu mtindo wa kuvusha fedha nje na usafirishaji wa viwango vikubwa vya fedha zinazofichwa ugenini kinyume cha sheria.

Na kama wamedhamiria kweli kupambana na rushwa wanapaswa kuanza na walio katika ngazi za juu serikalini.

Mwandishi: Hashimu Gulana/IPS

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman