Matangazo
Anadaiwa kuvaa nguo hiyo 'isiyo ya heshima' alipohudhuria tamasha la msanii maarufu kutoka nchini Ufaransa, Agosti 7.
Kulingana na mwendesha mashitaka wa serikali Liliane, alivaa nguo zilizokuwa zikionyesha sehemu zake za siri.
Hatua aliyosema iliashiria ukiukaji wa maadili na tamaduni. Hatua ya kukamatwa kwake imeibua mjadala mkubwa nchini humo. Ili kujua zaidi, Lilian Mtono amezungumza na mwenzetu aliyeko mjini Kigali, Janvier Popote na kwanza amemuuliza mjadala mkuu ni upi?