Raia wanaoishi kwenye mpaka wa Katuna baina ya Uganda na Rwanda wamefurahia kufunguliwa tena kwa mpaka huo uliokuwa umefungwa kwa miaka mitatu. Hata hivyo bado kuna masharti ambayo Rwanda imeweka kuhusiana na wale wanaotaka kuvuka kuingia nchini humo ikiruhusu tu raia wake wanaotokea Uganda, watalii pamoja na magari ya mizigo.