1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda yamuachia huru Paul Rusesabagina

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Rwanda imemuachia huru shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 25 gerezani kwa tuhuma za ugaidi.

https://p.dw.com/p/4PEip
Ruanda Paul Rusesabagina
Picha: Cyril Ndegeya/Xinhua/IMAGO

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo jana aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa amri hiyo ya rais ya kumuachilia Rusesabagina ilitolewa baada ya ombi lililotolewa kwa niaba ya Rusesabagina.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, Rusesabagina, aliyesifika kwa kuokoa maisha ya watu 1,200 katika hoteli aliyoisimamia wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994 baada ya kuachiliwa alikwenda moja kwa moja hadi kwenye makazi ya balozi wa Qatar mjini Kigali.

Anatarajiwa kuondoka Rwanda siku chache zijazo. Rais wa Marekani Joe Biden, ameipongeza hatua hiyo ya kuachiliwa Rusesabagina na kuzishukuru serikali za Rwanda na Qatar na maafisa wa Marekani waliohusika kufanikisha matokeo hayo aliyoyaita ya furaha.