Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC imetoa wito wa haraka kwa nchi wanachama kuchukua tahadhari zinazoshauriwa na wataalamu wa masuala ya afya ili kudhibiti kiasi kkikubwa cha maambukizi ya virusi vya corona kinachoshuhudiwa hivi sasa katika ukanda huo, huku ikiwataka viongozi kutunga sera na mikakati ya pamoja ili kudhibiti janga hilo. Hawa Bihoga alituandalia taarifa hii.