1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schalke zu schwach für Manchester

Sekione Kitojo27 Aprili 2011

Katika mchezo wa nusu fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya, Champions League,FC Schalke 04 ilikuwa nyumbani ikionyeshana kazi na Manchester United ya Uingereza,kazi ambayo ilikuwa pevu kwa Schalke 04.

https://p.dw.com/p/114Ru
Manuel Neuer mlinda mlango wa Schalke alijaribu kwa kila hali kuinyima ushindi Manchester lakini wapi!!!Picha: AP

Katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la mabingwa mabarani Ulaya Champions league, FC Schalke 04 ilikumbana na Manchester United ya Uingereza. Haikuwa kazi rahisi, na hatimaye mabingwa mara kadha wa ligi ya Uingereza, Premier League, katika msimu huu wamefungwa mabao watatu tu hadi sasa. Kwa upande mwingine Schalke 04 imeibuka mshindi mara zote ilipocheza nyumbani katika msimu huu wa Champions League.

Wataalamu, ambao waliipa Schalke 04 nafasi ya chini kuweza kuibika mshindi wa pambano hili dhidi ya Manchester United, wameweza kuthibitisha kile walichokiona. Schalke ilikuwa kwa muda mrefu ikifurukuta tu na kuonyesha woga na kuipatia Manchester nafasi kubwa ya kumiliki mpira. Timu hiyo ambayo hivi sasa inaongoza katika ligi ya Uingereza, Premier League ilipokea zawadi hiyo, na kuuendesha mchezo huo wanavyotaka na kufungua nafasi kadha. Karibu mchezo huo uwe kati ya Manchester United na mlinda mlango wa Schalke , Manuel Neuer. Kila mara mlinda mlango huyo ameonekana katika misukosuko kadha iliyoelekea langoni mwake na kuokoa. Hilo hata kocha wa Schalke Ralf Rangnik aliliona.

"Tumekuwa kwa robo saa tu ,kipindi cha kwanza ambapo , tulipata nafasi moja ama mbili nzuri , na kisha shambulizi moja ama mawili mazuri. Lakini baadaye, kadri muda ulivyozidi ndivyo tulivyozidi kurudi nyuma na kila nafasi ya waliyoipata ManU iliwafanya wajisikie kujiamini zaidi.

Hadi nusu ya kwanza ya mchezo kwisha matokeo yalikuwa 0-0, lakini baadaye mchezo uligeuka kuwa wa magoli. Manchester hawakuwa wakizitumia nafasi walizopata, na upande mwingine Schalke waliboronga kila walipojaribu kushambulia kwa kushutukiza, ama walishindwa kutoa pasi ya mwisho muhimu.

Baada ya saa nzima kwisha katika mchezo huo, hisia zilianza kuonesha kuwa Schalke wanaweza kurejea katika mchezo wao, lakini magoli yalikosekana. Kipigo mara mbili katika muda wa dakika tatu kupitia Ryan Giggs katika dakika ya 67 na Wayne Rooney katika dakika ya 70 kilizima moto wa Schalke kabisa. Mlinzi wa Schalke Christoph Metzelder alikuwa katika hali ya masikitiko makubwa.

Champions League Halbfinale Schalke vs Manchester
Christoph Metzelder mlinzi wa Schalke 04 akipambana na Wayne Rooney wa Manchester United ,katika pambano lanusu fainali ya Champions League.Picha: dapd

"Tulikuwa leo kiasi na mengi ya kuyafanya. Tulitaka kupambana kwa dhati, kuweza kupora mipira kila wakati kutoka kwa maadui, lakini baada ya muda fulani tulishindwa kabisa, na pia wenzetu walikuwa na ubora wa hali ya juu, wa kuweza kufanikisha kile wanachoweza, na kuweza kutuyumbisha huku na kule. Kwa kweli ni mara chache sana tuliweza kucheza vizuri".

Katika muda wa wiki moja, hapo May 4, kutakuwa na mchezo wa marudiano huko katika uwanja wa Old Traford mjini Manchester. Kwa Schalke ambao wako nyuma tayari kwa mabao 2-0, kuna nafasi tu ya kinadharia ya ushindi. Ndoto ya kuingia katika fainali ya kombe la mabingwa , Champions League kwa Wafalme hao wa bluu ,kama wanavyojulikana hapa, Ujerumani, Königsblauen , baada ya pambano hili ambalo hawakuoneysha kandanda safi , itabakia tu kuwa ndoto.

Mwandishi : Ziemons, Andreas / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: