1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuUjerumani

Scholz autembelea mji wa Magdeburg baada ya shambulio

21 Desemba 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani ameutembelea mji wa Magdeburg leo Jumamosi, saa kadhaa baada ya mwanaume mmoja kuvurumisha gari kwenye soko la Krismasi na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanne.

https://p.dw.com/p/4oSJu
Ujerumani Magdeburg 2024 | Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiwa kwenye eneo la mkasa
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiwa kwenye eneo la mkasa kwenye mji wa Magdeburg.Picha: Axel Schmidt/REUTERS

Shambulizi hilo kwenye mji huo wa katikati mwa Ujerumani limewajeruhi pia watu wengine wasiopungua 60.  Polisi inasema limefanywa na mshukiwa mwenye umri wa miaka 50, ambaye alihamia Ujerumani akitokea Saudi Arabia.

Inaarifiwa mwanaume huyo  anayefanya kazi ya udaktari alilielekeza kwa makusudi gari alilolikodi kwenye umati mkubwa wa watu uliokuwa umekusanyika kwenye soko la Krismasi la Magdeburg.

Mshukiwa huyo alikamatwa baadae na bado yumo kwenye mikono ya vyombo vya dola na taarifa za awali zinasema huenda alifanya shambulizi hilo peke yake.