Makala ya Sema uvume wiki hii Saumu Njama anaangazia utafiti uliofanywa nchini Uganda ambao umevumbua vifaa vya sensa vyenye uwezo wa kunakili hali ya hewa. Pia utasikia jini watafiti wa nchini Korea walio mbioni kuvumbua roboti yenye ngozi ya kuhisi mguso na kupona kutokana na uharibifu au majeraha.