Sensa ya wafanyakazi wa serikali yafanyika nchini DRC
4 Aprili 2013Matangazo
Kampeni ya sensa ya wafanyakazi wa serikali iliodhaminiwa na Afrika ya kusini imemalizika nchini humo. Serikali ya Kongo imeelezea kwamba ilikuwa ikipoteza kila mara dola milioni 20 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa, baada ya kubadili mfumo wa malipo ambao hivi sasa unafanyika kupitia benki. Kwa sasa jumla ya wafanyakazi ni laki tatu na hamsini elfu, zaidi ya nusu miongoni mwao wakiwa wazee. Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo na ripoti kamili. Kuskiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Josephat Charo