1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul:Khofu bado yatanda Korea ya kusini.

25 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDI8

Korea ya Kusini imesema, inauhakika kuwa jirani yake Korea ya Kaskazini inamiliki mabomu yasiyopungua mawili ya kinyuklia.

Waziri wa ulinzi Yoon Kwang-ing hata hivyo amesema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Korea ya Kaskazini inataka kufanya jaribio lake la kwanza la bomu la nyuklia.

Soeul hadi hivi sasa imesema kwamba Korea ya Kaskazini ina mpango wa kutengeneza silaha za kinyuklia.

Mapema mwaka 2005 Korea ya Kaskazini ilitangaza kuwa inamiliki silaha za nyuklia.

Marekani na Japan katika taarifa zao wamesema kuna wasi wasi kuwa hivi sasa Korea ya Kaskazini wanajitayarisha kufanya jaribio la bomu la nyuklia la chini ya ardhi.