SEOUL:Korea ya Kaskazini kusaidiwa mchele na Korea ya Kusini
22 Aprili 2007Matangazo
Korea ya kusini imekubali kuipa Korea ya Kaskazini tano mia 4 za mchele kuanzia mwezi ujao.
Lakini mchele huo utatolewa kama mkopo. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo baina ya wajumbe wa nchi hizo mbili za Korea juu ya ushirikiano wa kiuchumi.
Tamko lililotolewa baada ya mazungumzo hayo halikusema chochote juu ya tashi la Korea ya Kusini juu ya Korea ya Kaskazini kuanza kusimamisha mipango yake ya nyuklia.