1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Barnier wa Ufaransa yaangushwa bungeni

5 Desemba 2024

Serikali iliyodumu miezi mitatu chini ya Waziri Mkuu Michel Barnier nchini Ufaransa imeporomoshwa kwa kura ya kutokuwa na imani nayo bungeni jioni ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/4nlIe
 Michel Barnier
Waziri Mkuu wa Ufaransa Michel Barnier.Picha: Michel Euler/AP/picture alliance

Kura hiyo iliungwa mkono na wabunge wa mrengo wa shoto na mrengo mkali wa kulia, kwa wingi wa kura 331.

Vyama hivyo vilikerwa na hatua ya Barnier kutaka kutumia nguvu maalum za kikatiba kukwepa maamuzi ya bunge juu ya bajeti. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuondolewa madarakani kwa kura ya bunge tangu mwaka 1962.

Soma zaidi: Wabunge waiangusha serikali Ufaransa

Barnier, mwanasiasa mkongwe wa Kifaransa aliyejizolea umashuhuri kwa kuongoza mazungumzo ya Uingereza kujitowa kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit, aliteuliwa na Rais Emmanuel Macron kuwa waziri mkuu mnamo mwezi Septemba mwaka huu.

Rais Macron anatazamiwa kuhutubia taifa jioni ya leo na vyanzo vinasema huenda akamtangaza waziri mkuu mpya kabla ya Jumamosi.