1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Botswana yasifiwa kwa kukabidhi madaraka kwa amani

1 Novemba 2024

Botswana imepongezwa kwa namna inavyoendesha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani. Hii ni baada ya matokeo ya kushangaza ya uchaguzi ambayo yalivunja udhibiti wa miaka 58 wa chama tawala madarakani.

https://p.dw.com/p/4mV4L
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi
Rais wa Botswana Mokgweetsi MasisiPicha: MONIRUL BHUIYAN/AFP

Botswana imepongezwa kwa namna inavyoendesha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani. Hii ni baada ya matokeo ya kushangaza ya uchaguzi ambayo yalivunja udhibiti wa miaka 58 wa chama tawala madarakani.

Mwanasiasa mkongwe Mokgweetsi Masisi, mwenye umri wa miaka 63, ametangaza leo kuwa atakabidhi madaraka kwa mwanasheria wa haki za binaadamu Duma Boko mwenye umri wa miaka 54, katika siku zijazo baada ya kuporomoka kwa chama chake cha Botswana Democratic - BDP katika uchaguzi wa bunge Jumatano iliyopita.

Masisi alikiri kushindwa na akampongeza Boko kwa kuwa rais mteule. Boko, ambaye anaongoza chama cha Umbrella for Democratic Change - UDC alishindwa katika uchaguzi wa 2014 na 2019. Mkurugenzi wa Shirika la Wanasheria wa haki za binaadamu kanda ya Kusini mwa Afrika Washington Katema amesema ukweli kwamba rais alikuwa mwepesi kukiri kushindwa pia unadhihirisha sifa ya kidemokrasia ya Botswana, kama mojawapo ya nuru zinazoongoza katika uwanja wa demokrasia.