1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya DRC kusajili wanajeshi wapya

11 Oktoba 2012

Hali ya usalama ikizidi kuzorota katika eneo la Mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kutokana na makabiliano kati ya waasi na vikosi vya serikali, serikali imeamua kuwasajili wanajeshi wapya hasa vijana.

https://p.dw.com/p/16Nkp
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya KongoPicha: Reuters

Hata hivyo operesheni hiyo inaonekana kusuasua kutokana na vijana waliojiandikisha baadhi yao kuanza kutoroka makambini. Jeshi la Kongo linaonekana kuendelea kuwa na wanajeshi wengi waliofanya kazi chini ya utawala wa rais wa zamani wa Kongo, iliyokuwa ikijulikana kama Zaire wakati huo, Mobutu Sese Seko, ambao wengi wameshakuwa wazee. John Kanyunyu anatupia jicho harakati hizo za serikali ya Kongo kuwasajili wanajeshi wapya.

(Kuskiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi