1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Mseto yaundwa Sudan Kusini

22 Februari 2020

Sudan Kusini Jumamosi imefungua ukurasa mpya baada ya viognozi hasimu kuunda serikali ya mseto ambayo wafuatiliaji wengi wa hali nchini humo wanatumai itadumu.

https://p.dw.com/p/3YBs2
Südsudan Salva Kiir und Riek Machar | Entscheidigung für  Einheitsregierung
Picha: AFP/M. Kuany

Siku moja baada ya rais Slava Kiir kuivunja serikali iliyokuwepo, kiongozi wa upinzani Riek Machar aliapishwa kuwa makamu wa rais, muundo ambao ulishindwa kufanya kazi mara mbili na kuitumbukiza nchi hiyo kwenye mzozo wa vita uliowauwa karibu watu 400,000.

Sudan Kusini, taifa changa kabisa duniani ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 baada ya wafuasi wa Kiir na Machar kuingia kwenye makabiliano makali miaka miwili tangu iliposhinda harakati za kudai uhuru kutoka Sudan.

Mbinyo kutoka jumuiya ya kimataifa uliwezesha kupatikana kwa makubaliano ya amani ya mwaka 2018.

Katika kisa cha nadra kiongozi wa kania katoliki duniani Papa Francis aliibusu miguu ya Kiir na Machar na watolea wito wa kumaliza uhasama wakati walipomtembelea mjini Vatican mwaka uliopita.

Sherehe za kuundwa serikali mpya mjini Juba zilianza kwa viongozi hao kukabidhiwa picha ya tukio hilo ile iwe iwakumbushe wajibu walio nao.

Wasiwasi ulikuwa mkubwa

Symbolbild Stammeskämpfen im Sudan
Picha: picture-alliance/Photoshot/Xinhua/G. Julius

Wasiwasi kutoka Marekani, ambayo ni mchangiaji mkubwa wa misaada kwa Sudan Kusini na mataia mengine uliongezeka wakati Kiir na Machar waliposogeza mbele mara mbili muda wa mwisho uliowekwa kuudna serikali mwaka uliopita.

Hata hivyo chini ya wiki moja kabla ya muda wa mwishoni uliowekwa awamu hii mahasimu hao wawili walifikia makubaliano kwa kila upande kuwa tayari kulegeza misimamo kadhaa.

Kiir alitangaza uamuzi mgumu kuhusu suala tete la idadi ya majimbo na Machar aliridhia Kiir kushughulikia suala la ulinzi wake.

Siku ya Alhamisi walitangaza kufikia makubaliano ya kuunda serikali itakayoongoza kwa miaka mitatu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu, utakaokuwa wa kwanza tangu taifa hilo lilipopata uhuru.

Furaha kutoka kila upande

Südsudan - Referendum 2011 - Fahne
Picha: picture alliance/dpa/M. Messara

"Hatimaye amani iko mlangoni kwetu" ametangaza mwandishi habari wa kituo cha redio kinachofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Bor lililoathiriwa vibaya na mzozo nchini humo.

Kwenye eneo la Yambio, vijana waliobebea bendera wanaripotiwa kuteremka majiani kushangilia hatua hiyo.

"Ninafurahi pamoja na raia wa Sudan Kusini, zaidi wale waliopoteza makaazi, wasio na chakula na walio kwenye mateso waliosubiri kwa muda mrefu " ameandika Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Justin Welby kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nderemo na vifijo vilisikika muda mchache baada ya Machar kula kiapo na kumshukuru Papa Francis na wengine na kuahidi rais wa Sudan Kusini kwa kufanya kazi pamoja kukomesha mateso ya taifa hilo.