Baada ya serikali ya Tanzania kuonya kuhusu utoaji wa taarifa za maradhi vifo au wagonjwa bila kuzingatia misingi iliyowekwa, DW Kiswahili ilitaka kufahamu kwa undani tamko hilo la serikali limepokelewa vipi, na ikazungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, TLS, Dk. Rugemeleza Nshala, ambaye kupitia yeye, taasisi yao iliwahi kuzungumzia waziwazi kuhusu virusi vya corona. Sikiliza zaidi.