1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Israel lauwa waandishi watano wa Kipalestina

26 Desemba 2024

Shambulizi la Israel limewauwa waandishi watano wa Kipalestina nje ya hospitali moja katika Ukanda wa Gaza jana usiku. Hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya ukanda huo unaodhibitiwa na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4oaS3
Mashambulizi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat
Israel imekuwa ikifanya mashambulizi kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa GazaPicha: Saed Abu Nabhan/APA Images/ZUMA/picture alliance

Shambulizi hilo lilipiga gari nje ya hospitali ya Al-Awda katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa ukanda huo. Waandishi hao walikuwa wakifanya kazi na televisheni ya eneo hilo ya Quds News Network, ambayo pia iliripoti kuhusu shambulizi hilo.

Soma pia: Israel inaendeleza vita vyake dhidi ya wanamgambo katika Ukingo wa Magharibi

Jeshi la Israel limesema lilikilenga kikundi cha wapiganaji kutoka Islamic Jihad, wanamgambo wanaowaunga mkono Hamas. Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi Habari - CPJ inasema zaidi ya waandishi habari 130 wa Kipalestina wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo vilivyoanzishwa na shambulizi la Hamas Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israel.

Israel hairuhusu waandishi habari wa kigeni kuingia Gaza isipokuwa tu kama wanaongozana na jeshi lake.