Shangazi wa Rais wa Congo Joseph Kabila auwawa na mlinzi
15 Juni 2005Matangazo
Lubumbashi:
Shangazi wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amepigwa risasi na kuuwawa na mlinzi wake nyumbani kwake mjini Lubumbashi katika mkoa wa kusini mashariki wa Katanga. Esperance Kabila mwenye umri wa miaka 48 alikua akielekea chumbani jana usiku, pale mlinzi wake anayejulikana kwa jina la Kalulika alipompiga mguuni na kwenye ini. Kwa mujibu wa redio ya umoja wa mataifa OKAPI, mlinzi huyo ambaye ni jamaa wa marehemu amekamatwa na anahojiwa. Esperance Kabila ni mfanya biashara na dada wa Rais wa zamani Marehemu Laurent Desire Kabila ambaye pia aliuwawa na mlinzi wake Ikulu mjini Kinshasa 2001. Baraza la mawaziri likamteuwa mwanawe Joseph Kabila kuwa Rais.