Simba watatu wauawa katika mbuga ya Masai Mara
6 Oktoba 2020Matangazo
Vifo vya simba hao vinatokea wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la biashara ya nyama ya porini kufuatia janga la virusi vya Corona.
Kupitia ukurusa wao wa Facebook, kundi hilo la uhifadhi la Mara Predator Conservation limesema limesikitishwa na vifo vya simba hao watatu waliopewa majina ya Rafiki, Lenkume na mtoto wa kiume wa Lenkume.
Kundi hilo limeongeza kusema fisi wanne na swala mmoja pia walikufa baada ya kunaswa kwenye mitego 50 iliyogunduliwa na kundi hilo ndani ya mbuga ya wanyama pori ya Masai Mara.
Kumekuwa na ripoti kwamba kudorora kwa sekta ya utalii na ukosefu wa ajira uliosababishwa na janga la Covid-19 umesababisha ongezeko la visa vya ujangili kwa ajili ya kula au kuuza nyama ya porini.