Soko la mchele latarajiwa kufanyika kwa mikataba ya serikali
26 Julai 2023Soko la kimataifa la mchele linatarajiwa kufanyika kwa njia ya mikataba baina ya serikali za ulimwengu huku marufuku ya India ya bidhaa hiyo ikizidi kupunguza usambazaji wa mchele duniani. Marufuku ya India imesababisha wasiwasi juu ya usalama wa chakula. Waagizaji wa mchele sasa watalazimika kutafuta mikataba ya moja kwa moja na serikali husika katika uuzaji wa mchele nje ya nchi.
India yaamua kupiga marufuku usafirishaji nje ya nchi
India wiki iliyopita ilichukua uamuzi wa kupiga marufuku usafirishaji nje ya nchi mchele mweupe hatua ambayo imepunguza upatikanaji wa bidhaa hiyo kuu katika masoko ya dunia. Shirley Mustafa, mchambuzi wa maswala ya maso katika Shirika la Chakula na Kilimo cha Umoja wa Mataifa (FAO) amesema kuweka vizingiti vya ndani, katika mauzo ya nje kutapunguza imani katika biashara ya kimataifa.